Go back

Ombi La Wokovu

YAHUSHUA Mpendwa,

Nakukubali sasa kama BWANA na MWOKOZI wangu, Wewe ndiye Mungu ninayependa. Naamini ya kwamba ulilipa gharama ya dhambi zangu pale Kalvari, ulikufa na kufufuka katika siku ya tatu. Nauliza uje moyoni mwangu, nisamehe dhambi zangu, nioshe niwe msafi wa udhalimu wote. Pole kwa kutenda dhambi, na nageuka kutoka kwa dhambi hizo. Asante kwa kunijaza na Roho Mtakatifu wako, na kunipa hamu ya kukutumikia siku zote za maisha yangu, na uishi maisha yako ndani yangu YAHUSHUA, ili Utukuzwe! Asante kwa kunipa hamu ya kusoma Bibilia, na kunipa hekima niielewe. Asante kwa Kunipenda na Kuokoa roho yangu, ikisababisha Imani yangu kukua, ili siku moja nitakuwa na WEWE Mbinguni. Nijaze na Roho Mtakatifu wako sasa na niokoe kutoka kwa yule muovu katika jina lako YAHUSHUA Naomba! Nisaidie YAHUSHUA kukumbuka wote wametenda dhambi na kupungukiwa na Utukufu wa YAHUVEH, na ulikuja kutuokoa sisi watenda dhambi, ndio sababu wewe huitwa MWOKOZI wetu. Amina.

Soma ombi hili alafu isome tena, wakati huu BILA maarifa ya kichwa lakini na moyo wako wote, iamini kwa IMANI, na kumbuka YAHUSHUA SI Mungu Pekee, lakini YEYE ni rafiki wako wa dhati! Anakujali sana, Anakupenda sana. Jinsi vile ulivyo. Anachukia Dhambi, lakini Anakupenda WEWE, mtenda dhambi!

YAHUSHUA alilipa gharama ya dhambi zako, sasa hufai kujisikia kama mwenye hatia au aliyehukumiwa tena! Ungama dhambi zako kwa YAHUSHUA. Zitaje, alafu mwambie pole, muulize akusamehe! Dhambi zako zote za zamani na sasa. Dhambi ni kitu chochote ulichofanya au unachofanya kinchomchukiza YAHUVEH Mtakatifu. Hakuna mtu aliye bora zaidi kushinda mwingine! Kumbuka haya!

Soma Agano Jipya ili upate kujua YAHUSHUA ni nani. (Yohana 3:16) Bibilia husema lazima umwungame Yeye kama BWANA na Mwokozi ili Akuungame mbele yake Baba. Usione aibu kumjua YAHUSHUA, kwani Yeye HAONI aibu kukujua WEWE. Ambia mtu ya kwamba umemkubali YAHUSHUA wa Kalvari na Nazareti, siku hii na malaika wote mbinguni wanashangilia.

Turuhusu tushangilie nawe. Kama unahitaji Mchungaji, tuna wengi zaidi ya mmoja. Karibu katika Familia ya YAHUSHUA! TUNA MATUMAINI YA KWAMBA TUTAKUTANA NAWE MBINGUNI, KAMA SI HAPA DUNIANI!

Tuma Barua Pepe kwa Elisabeth na umueleze juu ya zawadi ya uzima wa milele ambayo umerithi kutoka kwa YAHUSHUA Masihi wetu Mpendwa!